Vitu Vidogo ni Muhimu Pia

Vitu Vidogo ni Muhimu Pia

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa. MATHAYO 7:7

Ni vigumu kwa nia zetu zilizo na kikomo kung’amua na kuamini kwamba Mungu anataka kuhusika katika vitu vidogo kabisa katika maisha yetu. Lakini usiwahi kusita kupeleka vile unavyofikiri ni vitu vidogo kwa Mungu. Hata hivyo vitu vyote ni vidogo kwa Mungu.

Ninakumbuka mwanamke aliyekuja kwangu kwa maombi na akataka kujua iwapo itakuwa sawa kwake kumwomba Mungu vitu viwili. Kama sivyo, alinihakikishia kwamba ataomba kimoja tu. Huwa ninahuzunika ninaposikia watu wakisema mambo kama hayo.

Tunaweza kushukuru kwa sababu Mungu ni mkarimu na anataka kutupatia hata zaidi kuliko vile tunavyojua kuomba. Hauna kwa sababu huombi (tazama Yakobo 4:2), kwa hivyo nenda uombe kwa ujasiri, kwa sababu ni mapenzi ya Mungu kwako kufany a hivyo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba hakuna sala ya ombi ambalo ni kubwa sana kwako…na hakuna sala ya ombi lililo dogo sana kwako. Leo, ninachagua kuleta kila hitaji la maombi na tangazo la shukrani kwako, hata liwe dogo au kubwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon