Sema kile Mungu anasema

Sema kile Mungu anasema

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Yoshua 1:8

 Mungu anatuambia kwamba wakati mwingi tunaotumia kutafakari na kunena Neno Lake, tutaona faida katika maisha yetu ya kila siku na hata kuwa na uhusiano wa karibu naye. Yeye hata anaahidi kwamba tutafanikiwa na kustawi! (Angalia Yoshua 1: 8.)

Ninaweza kushuhudia jambo hili kwa sababu nimepita majaribu mengi na hata nyakati za kudhoofisha kwa kuamini na kukiri Neno la Mungu juu ya maisha yangu.

Kuna jambo lenye nguvu linalofanyika tunapozungumza Neno lake kwa sauti kubwa. Ndivyo tunavyojifunza kwa makusudi kufikiria mawazo sahihi, hasa wakati tunapofanya maandiko yawe ya kibinafsi na ya imani.

Ni vizuri kusoma Neno na kulipokea ndani ya moyo wako, lakini unapokiri kwa sauti kubwa, unashiriki kikamilifu na kile ambacho Mungu anasema na kuachilia nguvu zake katika maisha yako. Ninawahimiza kutumia muda na kusoma na kutafakari juu ya Neno la Mungu, na kuweka mawazo yenu juu yake.

Lakini pia ninakuhimiza kuzungumza Neno. Unaweza kukata kauli kubadilisha maisha yako kwa kusema kile Mungu anasema. Soma Neno Lake na uliseme juu ya hali yako leo.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka kuachilia nguvu kamili ya Neno lako katika maisha yangu. Pamoja na kusoma na kutafakari juu ya Neno lako, ninachagua leo kulizungumza juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon