Wakati mambo mazuri yatatokea kwa watu ambao wamekuumiza

Wakati mambo mazuri yatatokea kwa watu ambao wamekuumiza

Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Mathayo 5:45

 Je! Umewahi kumwona mtu akipokea baraka kutoka kwa Mungu na ukahisi kama hawakustahili? Je! Umeona mambo mazuri yakitokea kwa mtu aliyekuumiza?

Wakati mtu aliyekukosea anapata baraka, inaweza kukuudhi … angalau ilinifanya hivyo mpaka nilipojifunza jinsi ya kusamehe. Biblia inasema kuwa mambo mema na mabaya hutokea kwa wenye haki na wasio na haki. Mtu aliyekuumiza akipokea baraka, inafanya kuwasamehe kuwa ngumu, lakini bado unaitwa kuwaombea.

Ninataka kukuhimiza leo kuwabariki watu ambao wamekuumiza kwa kuwaombea, hata kama unaweza kujisikia kuumizwa na kukasirishwa nao. Unapowaombea watu ambao wamekuumiza, ni chaguo unalofanya. Na msamaha unategemea uamuzi wako-si hisia. Lakini kuna uponyaji kwako. Maisha ya kusamehe husaidia kuwa zaidi kama Kristo. Unapojifunza umuhimu wa msamaha na kuanza kuomba kwa ajili ya baraka kwa wale waliokuumiza, moyo wako utaponywa kutokana na uchungu, na ukuaji wako binafsi utakuongoza kwenye baraka ambazo Mungu amepanga kwa ajili yenu.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, inaweza kuwa ngumu, lakini najua nahitaji kuomba na kuwabariki wale ambao wananiumiza. Ninatambua kuwa msamaha ni chaguo, kwa hiyo nakuomba unisaidie hata ninapoamua kusamehe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon