Wakati maendeleo ni ya polepole

Wakati maendeleo ni ya polepole

Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; Warumi 5:3

 Ni muhimu kufanya upya mawazo yetu, lakini ni muhimu kutambua kuwa mchakato huu wa kupangiliza au kufanya upya mawazo yetu utafanyika pole pole. Usivunjike moyo ikiwa maendeleo inaonekana polepole, au unapopungua au kuwa na siku mbaya. Inuka tena, jipige vumbi na uanze tena.

Wakati mtoto anajifunza kutembea, huanguka mara nyingi, kabla ya kukuza uwezo wa kutembea bila kuanguka; hata hivyo, mtoto huendelea. Anaweza kulia kwa muda baada ya kuanguka, lakini daima anainuka na kujaribu tena.

Kujifunza kubadili fikira zetu hufanya kazi kwa njia ile ile. Tunangángána na kuanguka, lakini Mungu daima yuko kutuchukua. Badala ya kukata tamaa, kumbuka kufanya kile ambacho Biblia inasema na “kushinda” katika shida yako, kwa sababu kwa vile unajitahidi ina maana unapigana vita vizuri vya imani.

Kutakuwa na siku ambazo hatuwezi kufanya kila kitu haki-siku ambazo mawazo yetu ni hasi. Lakini usiache kamwe kujaribu. Mungu, hatua kwa hatua anatuleta karibu na njia yake ya kufikiri, mradi tusikate tamaa!

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, asante kwa kunichukua ninapoanguka. Najua kwamba wakati ninajitahidi, Unaweza kufanya kazi ndani yangu kunisaidia kushinda mawazo yangu hasi na kunifanya zaidi na zaidi kulingana na Njia yako ya kufikiri.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon