Wewe Ndiwe Makao ya Mungu

Wewe Ndiwe Makao ya Mungu

Kila akiriye kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 1 YOHANA 4:15

Kama waaminio, tuna maisha ya Mungu ndani yetu. Sisi ndio makao au nyumba ya Mungu. Huu ukweli ni muhimu ili tufurahie ushirika wa karibu na wa ndani na Mungu. Mungu hufanya makao yake ndani yetu tukimpa Yesu maisha yetu, tukimwamini kama Mwokozi na Bwana wetu peke yake. Kutoka hapo, Mungu, kwa nguvu za Roho Mtakatifu, anaanza kazi ya ajabu ndani yetu.

Tunaweza kushukuru kwamba Mungu anatupenda na huchagua kufanya makao yake ndani ya mioyo yetu. Uteuzi huu hautegemei matendo yoyote mazuri ambayo tumefanya au ambayo tunaweza kufanya, lakini ni kwa neema, rehema, nguvu, na upendo wa Mungu peke yake. Kama waaminio ndani ya Kristo, tunakuwa makao ya Mungu (tazama Waefeso 3:17; 2 Timotheo 1:14).


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa vile unavyofanya makao ndani ya moyo wangu. Hauko mbali au usiyeweza kufikika. Ninakushukuru kwamba unaishi ndani yangu na unahusika katika kila eneo la maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon