Yesu Anafahamu Udhaifu Wako

Yesu Anafahamu Udhaifu Wako

Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi. WAEBRANIA 4:15

Neno la Mungu linafundisha kwamba Mungu anafahamu udhaifu wetu. Anauelewa kwa kuwa alivaa mwili wa kibinadamu ili ajitambulishe nasi, na alijaribiwa sawasawa na sisi. Na hata kama hakufanya dhambi, hastaajabu tunaposhindwa.

Ni sawa kuwa na udhaifu—ni ubinadamu. Huenda unauliza swali nililouliza nilipojaribu kuamini huu ukweli unaoweka huru: “Je, iwapo nitafikiri kuwa niko huru kuwa na udhaifu, haitanifanya kutenda dhambi zaidi?” Jibu ni hapana, hatakuwa hivyo.

Neema ya Mungu na uhuru inayotoa, haitushawishi kutenda dhambi zaidi, lakini hutushawishi kumpenda Yesu sana. Kadri tunavyotambua kwamba anatupenda tu jinsi tulivyo, ndivyo tunashukuru sana na kumpenda zaidi. Na huo upendo juu yake hutusababisha kutaka kubadilika kwa sababu inayofaa.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kipaji cha neema. Na asante kwamba unanipenda hata ingawa nina udhaifu na ushinde. Ninajua kwamba unanitia nguvu na kunifanya nifanane zaidi na Yesu. Ninashukuru kwa kazi yako, na ninakuamini katika kila hatua njiani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon