Acha Mungu Asaidie

Acha Mungu Asaidie

Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana maana pasipo mimi, ninyi hamwezi kufanya neno lolote. YOHANA 15:5

Kumekuwa na nyakati ambazo sisi wote tumewahi kujaribu kushughulikia hali zetu badala ya kumwamini Mungu kuzishughulikia kwa niaba yetu. Sio ishara ya udhaifu kukubali kwamba hatuwezi kujisaidia—ndio ukweli. Unaweza kufadhaika, kung’ang’ana na kukosa furaha kwa sababu tu unajaribu kufanya kitu usichoweza kudhibiti. Huenda unajaribu kubadilisha kitu ambacho Mungu peke yake anaweza kubadilisha.

Unapoendelea kumngoja Mungu kushughulikia hali hiyo, ninakuhimiza kushukuru kwamba Mungu yuko mamlakani na uamue kufurahia kungoja. Hilo linaweza kuwa gumu kwa kuwa linahitaji uvumilivu, lakini mwishowe huleta faida ya ajabu. Kumngoja Mungu humheshimisha, na Biblia inasema mtu anayemheshimu Mungu, naye atamheshimu pia (tazama 1 Samweli 2:30 Biblia).


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba sihitaji kukabiliana na hali yoyote mimi mwenyewe, lakini kwamba uko hapa kunisaidia. Ninapokungoja, nisaidie kufurahia mchakato huo, nikijua kwamba una mambo mazuri kwa ajili yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon