Kuomba katika jina lake

Kuomba katika jina lake

Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.  Yohana 16:23-24

Wakati mtoto wetu mdogo alikuwa bado shuleni, tulikuwa na watu ambao walikaa pamoja naye wakati Dave na mimi tulipokuwa tumesafiri. Ikiwa wale ambao walikuwa wakimtunza kwa kutokuwepo kwetu wangetaka kupata matibabu kwa ajili, tulipasa kutia saini hati ya kisheria ya kwamba wana haki ya kutumia jina letu kwa niaba ya mwana wetu-kwa kweli-kufanya maamuzi mahali petu.

Ndivyo Yesu alivyowafanyia wanafunzi Wake, na hatimaye, kwa wote ambao watamwamini. Alisema kwamba Mungu atajibu wakati tunapoomba kwa kutumia jina lake. Hii ni mamlaka wewe na mimi tumepewa kwa jina lake. Jina lake linachukua nafasi Yake-Jina lake linamwakilisha Yeye.

Tunapoomba kwa jina lake, ni sawa na kama ni Yeye alikuwa akisali. Pendeleo hili linaonekana ni ajabu sana kuamini! Lakini tunaweza kuamini kwa sababu tuna Maandiko ya kukubaliana na haya. Kwa hiyo tumia mamlaka ya jina la Yesu na uweke nguvu hiyo kufanya kazi ili kuushinda uovu na kuleta baraka za Mungu kwa ulimwengu huu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, naomba kwa ujasiri kwa jina la Yesu, nikijua kwamba Wewe unasikiliza na tayari kujibu. Asante kwa fursa nzuri ya kuomba kwa jina la Mwanao.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon