Acha Nuru Yako Iangaze

Acha Nuru Yako Iangaze

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.. MATHAYO 5:14

Kama waaminio ndani ya Kristo, tunaweza kububujika uzima. Tunaweza kuwa wenye msisimko, hai, wenye kujishughulisha, kuwa na nguvu, amani na kujaa furaha.

Utulivu na fikra zetu hutegemea vile tunavyomkaribia Mungu. Tunapomkaribia Mungu kwa ujasiri, kujaa shukrani kwa neema zake na kuamini kuwa anatupenda na yuko upande wetu, hatutakuwa na jingine ila kuwa na uzima tele tele. Lakini, kukamkaribia Mungu kidini na kwa kushikilia sheria, huiba maisha. Hakuyarutubishi. Kumbuka, Paulo alisema, “Kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2 Wakorintho 3:6). Wakati ule tunamfuata Roho, tunahisi kuhuishwa.

Kila mmoja wetu anafaa kujiuliza swali, Je, watu wanaweza kutaka nilicho nacho kwa kuyatazama maisha yangu na kuangalia utulivu wangu? Je, maisha yangu yanaakisi moyo wenye matarajio na shukrani, wenye kusisimka kuhusu yale Mungu anaenda kutenda kila siku mpya?

Sisi ndio tunafaa kuwa nuru ya dunia. Hakikisha nuru yako inaangaza zaidi leo.


Sala ya Maombi

Baba, nina shukrani tele kwamba sina lazima ya kukukaribia kwa kushikilia sheria, lakini ninaweza kuja kwa ujasiri kwenye kiti chako cha enzi kwa sababu ya neema zako za ajabu. Asante kwamba neema na furaha yako inaangaza maisha yangu na kuniruhusu kuwa nuru ambayo ulimwengu utaona.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon