Amini

Amini

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. —WAEBRANIA 11:6

Moyo wenye nia nzuri na unaoamini ni mmojawapo wa nia za roho ambazo ni muhimu sana katika uhusiano wetu na Mungu. Huenda hilo likachekesha, kwa sababu tunaitwa waaminiyo. Ni rahisi kufikiria kwamba waaminiyo wote huamini, lakini nimegundua kuna wengi walio na makusudio mema lakini ni “waaminiyo wasioamini.”

Katika Mathayo 8:13, Yesu anasema kwamba, na iwe kama unavyoamini. Si hilo wazo lina nguvu sana? Ni jambo la kupendeza kufikiria yale Mungu atafanya katika maisha yetu, iwapo tu tutaamini, anaweza…na ataweza. Kuamini ni uteuzi tunaofanya, na wakati wowote tunapoacha kuamini tunapoteza amani yetu na furaha. Unda desturi ya kuamka kila kila siku mpya ukisema kwa kurudia, “Ninaamini, ninaamini, ninaamini. Kwa usaidizi wa Mungu, ninaamini ninaweza kufanya chochote anachoweka mbele yangu.”

Unapojaribiwa kuwa na shaka, jikumbushe tu kwamba wewe ni aaminiye, na waaminio huamini wakati wote! Kuamini humpendeza Mungu na kuachilia kutimizwa kwa ahadi zake katika maisha yako.


Unapopoteza furaha na amani yako, chunguza kuamini kwako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon