Amini Mungu Huwa Anakusikia

Amini Mungu Huwa Anakusikia

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chochote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. —1 YOHANA 5:14–15

Katika Yohana 11:41-42, kabla Yesu amwite Lazaro kutoka kaburini, aliomba: “Baba, ninakushukuru kwamba umenisikia.” Maombi ya uhakika yalioje!

Shetani hataki uwe na uhakika wa aina hiyo. Lakini ninakuhimiza kuwa na uhakika unapoomba. Fanya uamuzi kwamba wewe ni aaminiye sio ombaomba. Nenda kwenye kiti cha enzi kwa jina la Yesu—jina lake litapata kushughulikiwa!

Kama wanadamu huwa tunafurahia kujua mtu maarufu na kuweza kutaja jina lake, tukitumainia kwamba litatupatia kibali na kutufungulia milango. Iwapo hilo hutusaidia kama wanadamu, hebu fikiria vile linatenda kazi hata vizuri katika maeneo ya mbinguni—haswa tukitumia jina lililo juu ya majina yote mengine—jina lililobarikiwa la Yesu!

Tunapoomba kwa jina la Yesu, tunampa Mungu kile chote Yesu alicho. Hilo linaweza kutupatia uhakika mkuu kwamba Mungu anasikia na kujibu maombi yetu.


Nenda kwa Mungu katika maombi—kwa ujasiri. Kwa matumaini. Katika jina la Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon