Angalia kutoka mahali ulipo

Angalia kutoka mahali ulipo

Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo. —Mwanzo 13:14

Inaonekana kwamba maisha daima ina njia zake za kutuleta mahali ambapo tunahitaji kuwa na mwanzo mpya.

Katika Biblia, Abramu alijikuta mahali hapo wakati Loti mpwa wake alichagua ardhi bora zaidi katika eneo hilo, akiwaacha Abramu na nchi isiyofaa sana. Lakini Mungu hakumuacha Abramu.

Badala yake alitokea na akampa Abramu maono mapya.

Ninapenda kile Bwana alimwambia Abramu baada ya yeye na Loti kutengana. Akamwambia, ” Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo..”

Ni maneno hayo, “angalia kutoka mahali ulipo”, ambayo ninasisitiza. Hiyo ni hatua ya mwanzo mpya … kuanza upya. Mungu mwenyewe atatuleta kwa wakati huo mara kwa mara.

Unaweza kuwa katika wakati huo sasa. Labda unataka kuvunja tabia mbaya au kufufua ndoto iliyopotea. Labda unataka kushughulikia juu ya fedha zako, kuanza biashara yako mwenyewe, kuandika kitabu … chochote kile, na Mungu anaweza kukuambia uanze sasa. Hii inaweza kuwa mwanzo wako mpya!

Baada ya Mungu kumwambia Abramu kuangalia kutoka mahali hapo, jambo lile alimwambia lilikuwa, “Simama, tembea katika nchi kwa urefu wake na upana wake, kwa maana nimekupa” (Mwanzo 13:17).

Mungu anaweza kukuambia sasa hivi uamke na kuendelea na ndoto yako au maono … kazi yako … maisha yako, kwa sababu Yeye amekupa. Sehemu yako ni kuendelea kutembea

Fanya kile unachohitaji kufanya. Inaweza kuwa si rahisi. Inaweza kuchukua muda. Lakini mwamini Mungu na uendelee kufanya kile unachohitaji kutenda. Angalia mahali ulipo sasa-na uendelee mbele!


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, bila kujali kilichotokea katika siku za nyuma, nisaidie kuangalia juu kutoka hapa nilipo. Ninakushukuru kwa mwanzo wako mpya kwa ajili yangu. Mimi nitaingia kwa ujasiri ndani yake na kutembea kwa ujasiri sawia na wito wako kwa ajili yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon