Mpango kamili wa Mungu kwako

Mpango kamili wa Mungu kwako

Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; Wafilipi 1:6

“Mungu ana mpango kamili wa maisha yako!” Sote tumeskia kauli hiyo, lakini sidhani wengi wetu wanaamini kweli. Labda ni neno “kamilifu” ambalo hutuvunja. Hakuna mtu aliye kamili, na wazo la kuwa mkamilifu linaongeza shinikizo na shida kwa maisha yetu.

Ukamilifu hauonekani kuwezekana. Lakini wajua nini? Inawezekana! Mpango wa Mungu si kamili kwa sababu sisi ni kamilifu. Mpango huo ni kamilifu kwa sababu Mungu ndiye Yeye aliyeuumba. Ukamilifu hutoka kwake, naye ndiye pekee aliye mkamilifu. Anatujua vizuri zaidi kuliko vile tunajijua wenyewe, na ameunda na kuweka hatua katika mpango ambao umetengenezwa kwa maisha yetu.

Paulo anatuambia katika Wafilipi 1: 6 kwamba Mungu alituokoa na kuanza kazi nzuri ndani yetu, na kazi Yake ndani yetu itafikia ukamilifu.

Tunapofikiri juu ya Mungu kufanya kazi ndani yetu, tunapaswa kujikumbusha wenyewe kwamba kama sisi sio wakamilifu, Mungu ni mkamilifu. Hakuna chochote tunachoweza kufanya kitakachokuwa cha kutosha kukidhi ukamilifu wa Mungu. Yesu peke yake, aliye mkamilifu, ni mzuri wa kutosha. Na kwa sababu sisi tuko ndani ya Kristo, mpango kamili wa Mungu unawezekana kwetu!

OMBI LA KUANZA SIKU

Eh Bwana, najua kwamba mimi si mkamilifu, lakini nashukuru kwamba mpango wako kwangu unategemea ukamilifu wako, sio wangu. Asante sana kwa kuendeleza kazi nzuri ndani yangu. Ninakuamini Wewe kuikamilisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon