Baba Anajua Vyema

Baba Anajua Vyema

…Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. — WARUMI 12:2

Kutakuwa na nyakati katika maisha yetu ambapo Mungu atataka tufanye kitu ambacho hatuelewi au kukubaliana nacho. Anapofanya hivi ni kwa sababu ana kitu kizuri akilini mwake kwa ajili yetu. Njia zake ziko juu ya zetu, na siku zote yeye ndiye huwa mwema kabisa.

Mungu anapotaka tufanye kitu ambacho ni kinyume cha mapenzi yetu, tunaweza kukumbuka maneno ya Yesu: “… Si mapenzi yangu bali (kila wakati) yako yatendeke” (Luka 22:42). Haya maneno si rahisi kuomba, lakini huwa yanaleta faida kubwa wakati wote katika maisha yetu. Tukitaka kitu, mara nyingi huwa hatukati tamaa kwa urahisi. Huchukua imani kubwa na kuvunjika ili kufika mahali ambapo tunahiari kusema, kama Yesu, si mapenzi yangu, bali yako yatendeke kila wakati.

La muhimu ni kwamba Mungu ana mpango mkuu juu ya maisha yetu, lakini huo mpango huhitaji kwamba tumfuate bila masharti. Huenda akakwambia utoe vitu ambavyo hutaki kuachana navyo. Huenda akakuambia uende mahali, ufanye vitu, au kukabiliana na watu ambao ni wagumu kwako. Huenda akakwambia unyamaze katika hali zingine na uongee katika zingine. Lakini chochote Mungu akwambiacho, kifanye na utulie kwa kujua kwamba, utiifu wako unakuleta karibu na naye.


Chagua kuweka mapenzi ya Mungu kabla ya mapenzi yako kila wakati.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon