Bure Umepokea, Bure Toa

Bure Umepokea, Bure Toa

Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
Yesu akamwambia, sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. —MATHAYO 18:21–22

Sijui kukuhusu, lakini nina furaha kwamba Mungu haweki mipaka kwa idadi ya nyakati ambazo atatusamehe. Bila kujali ni mara ngapi tutakosea na kupungukiwa, huendelea kutudhihirishia upendo wake kwetu kwa kutusamehe na kutukaribisha mara kwa mara tena.

Lakini si inashangaza vile tunavyohiari kuendelea kupokea msamaha kutoka kwa Mungu, ilhali tunataka kuwapa wengine msamaha kidogo? Tunakubali rehema bure, ilhali inashangaza vile tunaweza kuwakabili wengine kisheria, kuwa wagumu na kukosa huruma.

La muhimu ni hili: Kama watu ambao tumesamehewa mengi, ni muhimu kujifunza kuwapa wengine huohuo msamaha. Hatuwezi kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu huku tukiwa na uchungu, chuki na kutokusamehe mtu mwingine. Hii ni minyororo itakayotufunga kiroho na kutuweka mbali na mema ya Mungu katika maisha yetu.

Iwapo kuna watu ambao wamekudhuru na unapata ikiwa vigumu kuwasamehe, kumbuka tu vitu vyote ambavyo Mungu amekusamehe. Ukiutazama hivyo, msamaha unakuwa kitu rahisi cha kuwapa wengine.


Neema ya Mungu hutusaidia kufanya kwa urahisi vitu ambavyo vingekuwa vigumu kufanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon