Uaminifu huzidi ukamilifu

Uaminifu huzidi ukamilifu

lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. 2 Wakorintho 4:2

Tunaweza kujali sana juu ya kile ambacho watu wanatufikiria mpaka ambapo inatushusha kabisa na tuogope kuonekana vibaya. Lakini unajua nini? Nadhani ikiwa tutakuwa kweli zaidi, tutaweza kupata heshima zaidi kuliko sasa kwa kujaribu kujificha kila kitu, tukijifanya kuwa kamili. Ninaamini moja ya sababu kuu ambazo watu hupenda kunisikiliza ni kwamba nawaambia yale niliyojifunza kupitia matatizo yangu mwenyewe, udhaifu na makosa yangu. Inawasaidia kutulia, wanaelewana nami, na huwapa matumaini kwamba ikiwa naweza kufanya baadhi ya mambo niliyoyafanya na kufaulu hivyo, nao pia wanaweza.

Tunahitaji kuacha kuishi kwa hofu ya kufanya makosa, kwa sababu tutafanya makosa. Mungu hatuambii tusifanye makosa yoyote. Anatuomba tuwe waaminifu na wazi juu ya makosa yetu. Tunapojiweka wazi, Anaweza kutusaidia kujiondoa na kuendelea na vitu vingi na vyema. Usifiche makosa yako. Yaweke wazi ili uweze kujifunza kutoka kwayo. Unapoamini Mungu kwa uwazi na uaminifu, anaweza kukusaidia kushinda chochote.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nina udhaifu ambao nina aibu nao, lakini kuushikilia hakutanifanya vizuri. Ninachagua kuwa wazi juu ya makosa yangu ili uweze kunisaidia kuyashinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon