Idhini ya kuchangamka

Idhini ya kuchangamka

Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu. Zaburi 138:5

Nilikuwa mtu wa makali mno. Nilikuwa makali juu ya kile watoto wangu walivyofanya na jinsi walionekana. Nilikuwa na makali kuhusu jinsi nyumba yangu ilivyoonekana, jinsi nilivyotazama na kile ambacho watu walidhani. Nilikuwa makini juu ya kujaribu kumbadilisha mume wangu katika kile nilichofikiri anapaswa kuwa. Kwa kweli siwezi kutafakari kitu cho chote ambacho sikuwa na makali juu yake. Nilichohitaji kufanya ni kujipa idhini ya kuchangamka!

Sikujua jinsi ya kumwamini Mungu kwa maisha ya kila siku. Sikuwa na usawa karibu katika kila kitu. Sikuwa nimetambua kuwa kuchangamka na raha ni muhimu katika maisha yetu-hatuwezi kuwa na afya kiroho, kiakili, kihisia au kimwili bila hayo! Kwa kweli, furaha ni muhimu sana kiasi kwamba Mungu alihakikisha kuwa aliiweka katika Biblia. Anatuamuru kabisa tufurahi.

Zawadi bora unayoweza kutoa kwa familia yako na ulimwengu ni afya yako-na huwezi kuwa na afya bila furaha kuwa sehemu ya kawaida ya maisha yako. Leo, badilisha mazingira yako yote katika maisha yako na furaha. Jipe idhini ya kuchangamka!

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, usiache nikawa mkali sana. Nisaidie kukumbuka kujipa idhini ya kuchangamka na kusherehekea wema wako kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon