Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni watu matendo yake! 1 MAMBO YA NYAKATI 16:8
Mwanetu wa kiume alienda kwa huduma ya nje na timu ambayo hutembelea watu wasio na makao kila wikendi. Baada ya kusaidia katika huduma hii, alinipigia simu na kusema, “Nikiwahi kulalamika tena, tafadhali nipige na uniite mjinga!” Alishtuka kuhusu vitu alivyokuwa amenung’unikia awali mara tu alipoona watu wengine walivyokuwa wakiishi na kulinganisha na vile alivyoishi.
Tafakari kuhusu hilo: Wale ambao hawana mahali pa kuishi wangependa kuwa na nyumba ya kusafisha, huku tukilalamika kuhusu kusafisha nyumba zetu. Wangefurahia kuwa na gari waendeshe, huku tukilalamika kuhusu vile magari yetu yalivyozeeka. Ni rahisi kutoona vile tulivyobarikiwa, lakini tujaribu sana kuzipa fikra hizo kipaumbele. Shukuru kwa kile ambacho umebarikiwa nacho!
Chagua kumbariki Mungu wakati wote, bila kujali kinachoendelea, vile Daudi alivyosema: “Nitamhimidi Bwana kila wakati, sifa zake zi kinywani mwangu daima” (Zaburi 34:1).
Sala ya Shukrani
Ninashukuru, Baba, kwa baraka zako katika maisha yangu. Tafadhali nisamehe kwa nyakati ambazo nimepuuza wema wako na kuuona kama jambo la kawaida. Leo ninachagua kuwa na moyo wenye shukrani kwa kila baraka, hata kama ni ndogo vipi.