Chini ya Udhibiti wa Mungu

Chini ya Udhibiti wa Mungu

. . . [Bwana] hushusha chini tena huinua juu. —1 SAMWELI 2:7

Ni muhimu kukumbuka kwamba Bwana anaweza kushusha mtu mmoja na kuinua mwingine. Mfano mmoja uko katika maisha ya Esta. Mungu alimwiinua kutoka mahali pa taabu hadi kuwa malkia wa nchi nzima. Alimpa kibali mbele za kila mtu aliyekutana naye, pia mfalme, kwa sababu alikuwa amepata kibali mbele za Mungu.

Esta alitumia kibali hicho kujiokoa pamoja na watu wake, Wayahudi, kutokana na kuuawa na Hamani mwovu, ambaye alitaka kuwaangamiza. Huenda alikuwa mwoga wa kuenda kwa mfalme na kumwomba aingilie kati, kwa sababu kufanya hivyo kungemgharimu maisha yake mwenyewe, lakini alifanya hivyo kwa sababu alimwamini Mungu kwa ajili ya maisha yake.

Hali yoyote ikija katika maisha yako, hata kama unakasirishwa, kuteswa, au kubaguliwa au mtu anajaribu kuchukua kitu kutoka kwako ambacho ni chako kihaki—hata ikiwa ni kazi yako, nyumba yako, hadhi yako au kitu chochote maishani mwako—Amini Mungu atakupa kibali cha kimiujiza. Hata kama mambo yatakuwa ya kutamausha, Mungu anaweza kukuinua au kukushusha. Maisha yako yakiwa mikononi mwake, amini kwamba nuru ya Bwana huangaza juu yako ili kukupa kibali.

Usiishi maisha ukiwa na woga; Mungu anakupenda na atakusaidia kila wakati!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon