Daraja badala Ya Kuta

Daraja badala Ya Kuta

Kwa sababu ndio mlioitwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. —1 PETRO 2:21

Badala ya kuta nilizokuwa nikijenga kuzunga maisha yangu, nimejifunza kujenga daraja. Kwa nguvu za neema na msamaha wa Mungu, dhiki na vitu vibaya vilivyofanyika katika maisha yangu viligeuzwa na kuwa barabara kuu ambazo wengine wanaweza kupitia ili kupata uhuru niliopata.

Mungu hana upendeleo (Matendo ya Mitume 10:34). Kile amenitendea, anaweza kukutendea pia. Unapomkaribia Mungu kila siku, unaweza kutambua uhuru huohuo ambao nimepata, na unaweza kuwa daraja ya wengine kupitia, badala ya ukuta unaowafungia nje.

Yesu alituanzishia njia ya kwenda kwa Mungu. Amekuwa barabara kuu ya kupitia. Alijitoa dhabihu kwa ajili yetu, na sasa kwa kuwa tunafaidi kutokana dhabihu yake, anatupatia nafasi ya kujitoa dhabihu kwa wengine ili wavune faida hizohizo tunazofurahia.

Badala ya kufungia watu nje, ninapendekeza umwulize Mungu akuruhusu kuwaona vile unavyowaona. Wapende, wasamehe, na uwaelekeze kwa Mungu ili awaponye majeraha yao na kuwajaza amani na furaha.


Kuna watu waliopotea na wanahitaji watu kuwatangulia na kuwaonyesha njia. Kwani nini usiwe huyo mtu kwa ajili yao?

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon