Endelea Kuamini Mungu

Lakini yeye aijua njia niendayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. —AYUBU 23:10

Wakati wote kutakuwa na hali katika maisha ambapo tutahitajiwa kumwamini Mungu bila kujali kinachofanyika au hata kama hatuelewi kinachofanyika. Ndiyo kwa sababu mara nyingi huwa tunajipata tukimwambia Mungu, “Ni nini kinaendelea katika maisha yangu? Unafanya nini? Nini kinafanyika? Sielewi” Wakati mwingine vitu vinavyofanyika ndani yetu vinaonekana kutupeleka upande mkabala wa ule tunaohisi kwamba Mungu ametufunulia hivi karibuni.

Huu ndio wakati ambao watu wengi hukata tamaa na kurudi kufanya kitu ambacho kitakuwa cha upesi na rahisi kwao kufanya. Iwapo huku mahali katika maisha sasa hivi ambapo hakuna kitu kinaleta maana katika maisha yako, endelea kuamini Mungu. Yuko karibu nawe. Hajakuacha. Atakufanikisha.

Hakuna kitu kama kumwamini Mungu bila maswali ambayo hayajajibiwa. Mradi tu Mungu angali anatufundisha kumwamini, wakati wote kutakuwa na mambo katika maisha yetu tusiyoyaelewa tu. Mbingu linaponyamaza, endelea kufanya vitu ulivyojifunza na kujua kuvifanya, na uendelee kumwamini. Mungu atafanya vipande vyote vya maisha yako vifanye kazi pamoja kwa kusudi lake.


Mara nyingi majibu ya kesho hayaji hadi kesho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon