Endelea Kusonga Mbele

Endelea Kusonga Mbele

Umngoje Bwana, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje Bwana. ZABURI 27:14

Iwapo tutaenda kumfanyia Mungu kitu chochote kikubwa, na iwapo tumedhamiria kutokata tamaa kuhusu ndoto zetu, lazima tujaribu, lazima tuwe wajasiri. Tunapokabiliana na hali ambazo zinatutisha au kutuogopesha, tunahitaji kuomba kwa ajili ya ujasiri na roho shupavu. Kuhisi hofu sio shida bora tu tuwe na ujasiri mwingi kuliko hofu!

Roho ya hofu itajaribu kutuzuia kusonga mbele wakati wote. Kwa karne nyingi adui ametumia hofu kujaribu kukomesha watu, na habadilishi mkakati huo sasa hivi. Lakini shukuru, tunaweza kushinda. Sisi tu zaidi ya washindi kupitia kwake anayetupenda (tazama Warumi 8:37). Kutokuwepo kwa hofu si ujasiri; ni kuchuchumilia mbele huku hisia ya hofu ikiwepo. Unapohisi kuogopa, muombe Mungu kukutia nguvu, shukuru kwamba atafanya hivyo, na uchuchumilie mbele katika nguvu zake!


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa kipaji cha ujasiri. Ninashukuru kwa ndoto ulizonipa na dhamira uliyonipa ya kuzifuatilia. Ninachagua kutokata tamaa dhidi ya ndoto ulizotia katika moyo wangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon