Endelea Kusonga Mbele

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo na ya moyo wa kiasi (2 TIMOTHEO 1:7)

Katika vitu vya kiroho, huenda tunasonga mbele au tunarudi nyuma. Tunakua au kufa. Hakuna kitu kama ukristo uliolala au usiopendelea upande wowote. Hatuwezi kusitisha au kuhifadhi safari yetu ya ukristo hadi baadaye. Ni muhimu kuendelea kusonga mbele. Ndiyo kwa sababu Paulo alimuagiza Timotheo kuchochea karama ya Mungu iliyokuwa ndani yake na kuwasha moto wa Mungu katika moyo wake (soma 2 Timotheo 1:6).

Ni wazi kabisa kwamba Timotheo alihitaji himizo hili. Kwa mujibu wa andiko la leo, huenda alikuwa akipambana na hofu. Wakati wowote tunaporuhusu woga kutushika, tunadumazwa badala ya kushughulika. Hofu hutugandisha mahali; huzuia maendeleo.

Pengine Timotheo aliogopa kwa sababu wakristo wakati huwa walikuwa wakiteseka sana. Isitoshe, mshauri wake Paulo alikuwa ametupwa gerezani na huenda alikuwa akiwaza kuwa jambo hilo litamfanyikia pia.

Hata hivyo Paulo alimhimiza kujichochea, kuendelea na safari, kuwa mwaminifu kwa mwito wa Mungu juu ya maisha yake na kukumbuka kwamba Mungu hakumpa “roho ya woga, bali ya nguvu, na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”

Hiki haswa ndicho tunachopata tunapopokea ukamilisho wa Roho Mtakatifu- nguvu, upendo, na moyo wa kiasi. Unapojaribiwa kuogopa , kukumbuka ukweli huu. Jitenge peke yako na Mungu na uache Roho Mtakatifu akujaze ujasiri na uhakika ili uweze kusonga mbele.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Hakikisha una ushirika na Yesu leo na sio na shida zako; fikiria kumhusu, usifikirie shida zako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon