
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. WARUMI 14:17
Mtu mwenye hekima huwa haruhusu hisia za mtu mwingine kubadilisha zake.
Kuna kisa cha mwanamume Mquaker ambaye alikuwa anatembea barabarani na rafiki yake aliposimama kununua gazeti katika kibanda cha habari. Mwenye duka alikuwa mjeuri sana ambaye hakuonyesha urafiki. Mwanamume huyo Mquaker alimjibu kwa heshima na alikuwa mpole katika vile alivyomshughulikia. Baada ya kulipia gazeti lake na kuendelea na mwendo wao, rafiki yake aliuliza, “Ungekuwaje tu mpole kwa huyo mwanamume haswa ukikumbuka vile alivyokufanya?” Mwanamume Mquaker akajibu, “Eh, yeye huwa tu hivyo; kwa nini nimwache kuamua vile nitakavyotenda?”
Hii ni mojawapo ya sifa za ajabu ambazo tunaona ndani ya Yesu—alibadilisha watu, hawakumbadilisha. Ninakuhimiza kufuata mfano wa Yesu. Fanya kile Mungu anatarajia ufanye na usiishi chini ya utawala wa hisia na fikra za watu.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kuwa ninaweza kuwa na furaha katika kila hali. Leo, ninachagua kutowaruhusu watu wengine kuamua nitakavyoishi. Kwa usaidizi wako, nitaishi kwa furaha bila kujali hali zinazonizunguka.