Furaha Tele Tele

Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako wa kuume mna mema ya milele. —ZABURI 16:11

Uwepo wa Bwana huwa nasi wakati wote, lakini huwa hatuutambui au hata kuchukua muda kufikiria kuuhusu. Ninafikiri ndiyo kwa sababu inaonekana kuna ukosefu wa furaha katika maisha ya waaminio wengi. Kuna watu wengi wasio na furaha ambao wanaishi maisha yao kwa kufukuzana na vitu, ilhali hakuna kinachoweza kuturidhisha isipokuwa Mungu mwenyewe.

Watu wanapokosa kuridhika ndani ya mioyo yao, huwa mara nyingi wanatafuta kitu nje cha kuridhisha njaa yao. Mara nyingi huwa wanaishia kutafuta kile ambacho hakiwezi kujaza utupu wa ndani. Tumesikia ikisemwa watu wengi huishi maisha yao wakijaribu kupanda ngazi ya mafanikio, na kugundua tu kwamba wakishafika juu, ngazi yao imeegemea mjengo usio sawa.

Tukijua mambo yanayofaa kufanywa kwanza, tunagundua kwamba kila kitu ambacho kwa kweli tunahitaji maishani kinapatikana ndani ya Mungu. Tafuta kuishi katika uwepo wake. Ndani yake, mna njia ya uzima, furaha tele tele, na raha milele na milele.


Sababu ya kucheka kwetu na kufurahia maisha bila kujali hali tulizo nazo, ni kwa sababu Yesu ni furaha yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon