Hakuna Kutojiamini Tena

Hakuna Kutojiamini Tena

Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake, lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. —1 SAMWELI 30:6

Tukikosa kujiamini—katika talanta na uwezo ambao Mungu ametupatia—ni nani atakayetuamini? Mungu anatuamini, na kitu chema pia; la sivyo huenda tusipige hatua yoyote. Hatuwezi kila mara kungoja mtu aje na kutuhimiza tuwe kila tunachoweza kuwa.

Daudi na wanaume wake walipojipata wakiwa katika hali iliyoonekana kukatisha tamaa, ambayo wanaume hao walimlaumu kwa hiyo hali, Daudi alijihimiza na kujitia nguvu katika Bwana. Baadaye, hali hiyo ikabadilishwa kabisa (1 Samweli 30: 1-20).

Daudi alipokuwa mvulana tu, kila mtu karibu naye alimkatisha tamaa kuhusu uwezo wake wa kupigana na Goliathi. Walimwambia alikuwa mdogo sana na asiyekuwa na tajriba, na hakuwa na silaha zilizofaa. Lakini Daudi alikuwa karibu na Mungu na alikuwa na ujasiri ndani yake. Daudi aliamini kwamba Mungu ataonyesha nguvu kwa niaba yake na kumpa ushindi.

Kujishuku hutesa sana, lakini tunaweza kujiepusha na shaka. Kama Daudi, tunaweza kujifunza kumjua Mungu wetu—kuhusu upendo wake, njia zake na Neno lake—halafu mwishowe tunaweza kumtumainia kwamba atatupa nguvu tunazohitaji.


Njia ya kukomesha mateso ya kujishuku ni kumtazama Mungu na kuwa na imani katika uwezo wake mkuu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon