Hataacha Uzame

Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu. —YUDA 24

Watoto wengi ambao bado wanajifunza kuogelea huwa na woga wakiwa bwawani. Isipokuwa wawe wamebebwa na wazazi wao au mtu mwingine mzima wanayemwamini, huwa na hisia za kukosa usalama kwa sababu huwa wanagundua kwamba maji yako juu ya vichwa vyao.

Katika maisha yetu, mara nyingi sisi wote huogopa kwamba tunaingia ndani “juu ya vichwa vyetu” au tunahisi tuko “nje ya lindi letu.” Ukweli ni kwamba, bila Mungu, huwa tuko ndani juu ya vichwa vyetu wakati wote. Kuna matatizo na changamoto zinazotuzingira katika maisha. Zingine ni ndogo na zinazotutaabisha; zingine ni kubwa na za kututisha. Gari linaharibika, unasimamishwa kazi, rafiki au jamaa anafariki, ubishi unatokea, ripoti mbaya inakuja kutoka kwa daktari. Vitu hivi vinapofanyika, ni rahisi kushtuka kwa sababu tunahisi tuko ndani juu ya vichwa vyetu.

Lakini ukweli ni kwamba, hatujawahi kuwa katika usukani kwa kweli tukija kwenye vipengele muhimu vya maisha. Tumekuwa tukitegemea neema ya Bwana kutupitisha katika hali zote. Mungu hajawahi kuwa nje ya lindi lake. Tukimtegemea, tunaweza kutulia na kuwa na amani, tukijua atatupitisha katika hali zote. Hatatuacha tuzame.


Uko salama mikononi mwa Baba yako. Hata kama utahisi uko ndani juu ya kichwa chako, anakushikilia kwa neema yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon