Moyo wa mtu huifikiri njia yake; bali Bwana huziongoza hatua zake. MITHALI 16:9
Mara nyingi, tunafanya mpango halafu tunauombea ili ufanye kazi. Lakini Mungu anatutaka tuombe kwanza na tumwulize mpango wake. Halafu baada ya kuwa na mpango wake, anataka tuamini kwamba atautimiza. Tunaweza kuishi na moyo wa sifa na shukrani, tukijua kwamba mipango ya Mungu hufanikiwa wakati wote.
Shughuli zilizozalishwa kutokana na mwili, jitihada zetu bila Mungu, kwa kweli huzuia nguvu za Mungu kudhihirika katika maisha yetu. Biblia inaeleza shughuli hizo kama “kazi za mwili.” Nimekuja kugundua kwamba kazi za mwili ni “kazi zisizofanya kazi.” Hivyo sivyo jinsi ya kuishi maisha ya juu ambayo Mungu ametuandalia. Omba kwanza, mwulize Mungu mpango wake, na umwamini kufanya kazi katika maisha yako.
Sala ya Shukrani
Baba, asante kwa kipaji cha maombi. Badala ya kuegemea ufahamu wangu leo, nitakuja kwako kwanza na kukuuliza unionyeshe mpango wako juu ya leo na juu ya maisha yangu.