Hicho Kitu Kimoja Kisichoshindwa

Hicho Kitu Kimoja Kisichoshindwa

Upendo huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wowote; bali. . . —1 WAKORINTHO 13:7– 8

Upendo wa Mungu huvumilia yote yanayokuja. Huvumilia kila kitu bila kufifia. Hudhamiria kutokataa tamaa hata kitu gani kifanyike. Hata mtu sugu ambaye huendelea katika uasi anaweza hatimaye kuyeyushwa kwa upendo. Biblia inasema, “… wema wa Mungu hukuvuta upate kutubu” (Warumi 2:4) Ni upendo wa Mungu—Wema wake na huruma—ambavyo vinaweza kubadilisha moyo.

Ninaelewa ni vigumu kuendelea kuonyesha upendo kwa mtu ambaye haukubali au hata kuupokea. Ni vigumu kuendelea kuonyesha upendo kwa wale watu ambao huchukua kutoka kwetu vyote tunavyohiari kutoa, lakini ambao hawatoi chochote vilevile. Lakini hatuwajibikii matendo ya watu wengine, ila tu tunavyotenda sisi wenyewe.

Tumeishi katika upendo wa Mungu kwa rehema zake, na sasa anatuagiza kuuonyesha ulimwengu aina hiyo ya upendo. Thawabu yetu haitoki kwa binadamu, lakini kutoka kwa Mungu. Hata matendo yetu mazuri yasipotambuliwa, Mungu hutambua na kuahidi kututuza hadharani kwa ajili yao (Mathayo 6:4). Iwapo utaamua kuonyesha upendo wa Mungu kwa wale ambao wamekuzunguka, hawatabarikiwa tu peke yao, Mungu atahakikisha kwamba pia nawe umebarikiwa.


Mungu ni upendo, na upendo huwa hauchoki.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon