Hicho “Kitu Kitakatifu”

Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia  juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu (LUKA 1:35)

Bikira Maria akachukua mimba kwa nguvu za Roho Mtakatifu , ambaye alimjilia juu yake, kulingana na andiko la leo, tumboni mwake, “kitu kitakatifu” kikapandwa. Roho wa utakatifu alipandwa ndani yake kama mbegu. Katika tumbo lake hiyo mbegu ilikua na kuwa Mwana wa Mungu na Mwana wa binadamu, ambaye alikuwa muhimu kwa ukombozi wa watu kutoka dhambini.

Tunapozaliwa mara ya pili, nguvu kama hizo hufanyika ndani yetu. Hicho “Kitu Kitakatifu,” Roho wa Utakatifu, anapandwa ndani yetu kama Mbegu. Tunapoinyunyizia maji ile Mbegu kwa Neno la Mungu na kuzuia “magugu ya anasa za ulimwengu” kulisonga na kuliondoa, litakua na kuwa mti mkuu wa haki, “miti ya haki iliyopandwa na Bwana ili atukuzwe” (Isaya 61:3).

Neno la Bwana hutufundisha kutafuta utakatifu (soma Waebrania 12:14). Tunapoweka mioyo yetu katika kuutafuta utakatifu, Roho wa utakatifu hutusaidia. Tukitaka kuwa watakatifu, tunahitaji kujazwa na Roho Mtakatifu na kumruhusu kuzungumza nasi, kuturekebisha, kutuongoza, na kutusaidia katika kila eneo la maisha yetu.

Usiwahi kukisahau hicho “Kitu kitakatifu” kinachoishi ndani yako. Inyunyizie mbegu hiyo Neno la Mungu na uache Roho Mtakatifu akuzungumzie na kukufundisha jinsi ya kuisaidia kukua.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Roho Mtakatifu anatamani kuwa mwenzi wako anapokufundisha na kukuelekeza katika utakatifu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon