Imani Haiuzwi

Imani Haiuzwi

…ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. —WARUMI 5:2

Shetani anataka mimi na wewe tufikiri kwamba tunaweza kununua neema ya Mungu kwa matendo yetu. Lakini neema ya Mungu haiuzwi, kwa sababu kwa ufafanuzi wake—kibali kisichostahili—ni zawadi.

Neema haiwezi kuchumwa kwa maombi, matendo mema, kusoma Biblia, kukiri maandiko, au kwenda kanisani. Haiwezi hata kununuliwa kwa imani. Neema ya Mungu hupokewa, lakini “hainunuliki.”

Hata tukifanya mambo yote mazuri, ni muhimu nia zetu kuwa safi. Tunapokuwa na ushirika na Bwana, kama nia yetu ni kupata kitu kutoka kwake, tumeoondoka kwa neema hadi kwa matendo. Hebu tusianguke kwenye mtego wa kufikiri kwamba tunastahili kitu chochote chema kutoka kwa Mungu. Wema wa Mungu ni zawadi na tunaweza tu kumshukuru na kujawa na shukrani. Kitu chochote kinachofanyiwa Mungu kifanywe kwa sababu tunampenda, na sio kupata kitu chochote kutoka kwake.

Tunaweza kumtafuta Bwana na kuwa na ushirika naye bila sababu yoyote isipokuwa tu kwamba tunapenda na tunataka kuwa karibu naye kila siku.


Wokovu na kila kitu kizuri kutoka kwa Mungu ni zawadi na hupokewa kwa imani peke yake, ili mwanadamu asijivune.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon