Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. MATHAYO 18:4
Imani ya mtoto ni rahisi. Mtoto huwa hajaribu kufikiria kila kitu na kufanya mpango wa kina kuhusu vile atakavyopata kabisa kile anachohitaji. Huwa anaamini tu kwa sababu wazazi wake walisema watamshughulikia.
Shukuru kuwa hilo ni la kweli kwetu sisi pia. Kama waaminio, furaha yetu na amani hazitegemei kufanya na kufanikiwa—katika kujaribu kufikiria na kufanya sisi wenyewe. Huja kwa kuamini.
Furaha na amani huja kama matokeo ya kujenga uhusiano wetu na Bwana. Zaburi 16:11 inatuambia mbele za uso wake ziko furaha tele. Iwapo tumempokea Yesu kama Mwokozi na Bwana, Yeye, Mfalme wa Amani, huishi ndani yetu (tazama 1 Yohana 4:12–15; Yohana 14:23). Huwa tunakuwa na amani katika uwepo wa Mungu, tukipokea kutoka kwake na kutenda kulingana n a anavyotuelekeza. Furaha na amani huja kutokana na kujua na kuamini—huku tukimwamini Bwana kwa imani rahisi kama ya mtoto.
Sala ya Shukrani
Ninashukuru kwamba furaha na imani yangu hazitegemei uwezo wangu. Baba, ni ndani yako ambamo ninapata kila kitu ninachohitaji. Leo ninakuja kwako kwa imani kama ya mtoto, nikiamini kwamba utashughulikia shida yoyote katika maisha yangu. Asante, Baba, kwamba unatawala maisha yangu, na amani na furaha yangu inapatikana ndani yako.