Imani Na Radhi

Imani na Radhi

. . . Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo. —WAFILIPI 4:11

Biblia inatufundisha kuridhika hata kama hali zetu ziko vipi (Waebrania 13:5). Si lazima tusikitike kuhusu chochote, hata kitu gani kikiwa kinafanyika. Badala yake, tunaweza kuomba kukihusu na kumwambia Mungu hitaji letu. Tunapomngojea kujibu, tunaweza kushukuru kwa yale ambayo Mungu ametutendea tayari (Wafilipi 4:6).

Nimegundua kuwa siri ya kuwa katika hali ya kuridhika ni kumwambia Mungu tunachotaka, kujua kwamba ikiwa ni kinafaa, atakifanya kitimie kwa wakati unaofaa. Na kama hakifai, atafanya kingine kilicho bora kuliko kile tulichomwomba.

Ni muhimu tujifunze kumwamini Mungu kikamilifu iwapo tunakusudia kufurahia amani tele katika kuishi kwetu. Tuna nafasi ya kutafakari kuhusu yale Mungu ametenda katika maisha yetu badala ya yale tunamngoja atufanyie.

Mungu anakupenda. Ni Mungu mwema ambaye anataka kuwa karibu nawe. Ridhika ukijua kwamba njia yake ni timilifu, na anakuja na thawabu kuu kwa wale wanaomwamini (Waebrania 10:35).


Mungu anafanya kazi kwa siri, kisirisiri, hata kama inaonekana kwamba hakuna kitakachowahi kubadilika.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon