Jibu Haliko katika Nyota

Msiwaendee wenye pepo wala wachawi msiwatafute ili kutiwa unajisi na wao, Mimi ndimi Bwana. (MAMBO YA WALAWI 19:31)

Kama waaminiyo, tunaweza kukaribia Mungu na ulimwengu wa kiroho. Tunaweza kusikia sauti ya Mungu na kupokea uelekezi kutoka kwa Mungu. Watu wengi wanataka uelekezi wa kiroho, lakini sio kila mtu anautafuta kutoka kwa Mungu.

Watu wengi ulimwenguni hutafuta ushauri na mwelekeo kutoka kwa nyota, mabingwa wa maono, wapiga ramli, na vitu kama hivyo na watu. Haya ni makosa na chukizo kwa Mungu. Shetani hudanganya watu wengi kupitia kwa njia hii. Watu wanatafuta maelekezo na suluhu kwa maisha yao, lakini la kuhuzunisha ni kwamba hawajafundishwa kwamba Mungu atawapa. Kusudi langu la kuandika ibada ya leo ni kuwajulisha kwamba Mungu anataka awe chanzo cha habari kwako. Anataka kukupa mwelekeo wa kila siku wa maisha yako kupitia kwa Neno lake na Roho wako.

Niliwahi kufanya kazi na mwanamke ambaye alihusika kiundani na unajimu. Alitafuta ushauri wa nyota kabla ya kufanya uamuzi wowote. Alichunguza pia mpangilio wa nyota kuangalia ile siku angenyoa nywele. Kwa nini tutafute ushauri wa nyota kama tunaweza kutafuta ushauri wa Mungu, ni nani aliyetengeneza nyota?

Iwapo unatafuta mwelekeo kutoka katika chanzo chochote isipokuwa Mungu, ninakuhimiza utubu, umgeukie, na kumwomba Roho Mtakatifu kuwa mwelekezi katika maisha yako kuanzia sasa.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Tafuta habari na mwelekeo kutoka kwa Mungu.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon