Msifu Mungu katika gereza lako

Msifu Mungu katika gereza lako

Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafla pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika,  na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Matendo ya Mitume  16:25-26

Wakati mwingine tunajikuta katika fujo mbaya sana kiasi kwamba ni vigumu kusubiri fursa kwa ajili ya kufunguliwa na kutolewa. Lakini tunahitaji kusubiri Mungu na kumtegemea kwa imani nzuri na rahisi. Kisha, kwa namna ambayo hatuwezi kamwe kuamua – Mungu hutokea kighafla!

Paulo na Sila walijua kuhusu kusubiri, nao walingojea vizuri. Matendo ya Mitume 16 inaelezea hadithi ya jinsi walivyoshambuliwa na umati, kupigwa na kutupwa jela. Mstari wa 24 unasema mlinzi wa gereza aliwaingiza gereza la ndani (shimoni) na akafunga miguu yao katika hifadhi. Paulo na Sila hawakuwa na wasiwasi-waliamua tu kuanza kuimba na kuanza kumwabudu Bwana. Walianza kumngojea Mungu.

Ghafla, Mungu alituma tetemeko la ardhi ambalo lilifungua milango ya gerezani na kufungua minyororo yao. Aliwaweka huru!

Wakati watu wanaposubiri kwa kutarajia na kumngojea Mungu katikati ya hali mbaya, ghafla Mungu hujitokeza. Basi usikate tamaa! Usiache kuamini! Endelea kwa ukamilifu na matumaini. Nguvu za Mungu hazipunguki, na Yeye atakuja kwa ajili yako

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, bila kujali jinsi maovu yangu yanavyonipata, ninakuchagua kukusifu katika gereza langu. Najua Wewe utakuja kwa ajili yangu, na Unaweza kutokea “ghafla” wakati uliofaa wa kunifungua.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon