Jifunze Kutokana na Maombi ya Paulo

Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye (WAEFESO 1:17) 

Ninataka kutazama baadhi ya maombi ya Paulo leo. Niliposoma maombi yake katika Waefeso, Wafilipi na Wakolosai, nilihisi vibaya kuhusu maisha yangu ya maombi ya kimwili, na maombi ya Paulo yakaniathiri kwa nguvu kiasi kwamba maisha yangu ya maombi hayajabaki yalivyokuwa. Niliona kwamba Paulo hakuwahi kuombea watu kuwa na maisha rahisi au kuondolewa kwa matatizo. Badala yake, aliomba kwamba waweze kuvumilia yaliyowafika kwa upole, subira, uvumilivu, na kuwa mifano ya watu wanaoishi kwa kuonyesha neema za Mungu kwa watu wengine. Aliomba kuhusu vitu vilivyo muhimu kwa Mungu, na ninaweza kukuhakikishia kutokana na tajriba, huachilia nguvu za ajabu tukiomba hivyo. Tunafaa kushughulikia hali yetu ya kiroho kuliko vile ambavyo huwa tunashughulikia vitu vyote tunavyotaka.

Andiko la leo ni mojawapo ya maombi ya Paulo. Andiko hili linatufundisha kuomba kwa ajili ya roho ya hekima na ufunuo- na hayo yanahitaji kuwa mojawapo ya maombi ya kimsingi. Kwa kweli, ninaamini kumwomba Mungu ufunuo- utambuzi wa kiroho na ufahamu- ni mojawapo ya maombi muhimu ambayo watu wanaweza kuomba. Ufunuo unamaanisha “kufunua,” na tunahitaji kumwomba Mungu kutufunulia kila kitu kilicho chetu ndani ya Yesu. Tunamhitaji kufunua na kuweka wazi ukweli wa Neno ili tuelewe jinsi ya kujiombea na kuombea wengine. Mtu akikuambia kuhusu kanuni ya kiroho au ukweli wa kiroho, hiyo ni habari tu. Lakini Mungu akikusaidia kuelewa, unakuwa ufunuo- na ufunuo ni kitu kinachofanya ukweli kuwa halisi kwako kiasi kwamba hakuna kinachoweza kuuchukua kutoka kwako.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jipumzishe kutokana na kumwomba Mungu vitu na badala yake uombe uwepo zaidi wake katika maisha yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon