Jinsi ya Kuwa na Furaha

Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadri ya neema mliyopewa… (WARUMI 12:6)

Kila mmoja wetu amepewa karama na kuneemeshwa kwa njia tofauti kufanya kazi katika karama ambazo Mungu alitupatia. Andiko la leo linasema tunafaa kutumia karama zetu kulingana na neema iliyo juu yetu.

Watu wawili wanaweza kupewa karama ya kufundisha, ilhali huenda mwingine akawa mwalimu aliyeimarika kuliko huyo mwingine kwa sababu yeye ana neema zaidi ya mwito huo kutoka kwa Mungu. Kwa nini? Kwa sababu Roho Mtakatifu hugawa karama kwa yeyote kama anavyopenda (soma 1 Wakorintho 12:11). Ana sababu zake za kutenda kama anavyotenda, na tunahitaji kumwamini katika hilo. Tunafaa kuwa na wingi wa shukrani kwa kile anachotupa na kutokuwa na wivu na karama ya mtu mwingine. Hatuwezi kutembea katika upendo na watu na kutamani karama zao wakati huo huo.

Mume wangu anaweza kuwa na wivu kwa kuwa Mungu amenipa karama ya kuhubiri ambayo hakumpa. Dave aligundua kitambo sana kwamba hatakuwa na furaha akifanya kazi nje ya neema aliyopewa. Akijaribu kuwa nilivyo mimi, atapoteza furaha yake. Dave amepakwa mafuta ya usimamizi na fedha, na jukumu lake katika huduma ni muhimu tu jinsi wangu ulivyo.

Ukitaka kuwa na furaha ya kweli, jipeane kwa kile ambacho umeitiwa na kuneemeshwa kufanya. Roho Mtakatifu atakuzungumzia kuhusu kile unachofaa kufanya na kukusaidia kuelewa neema uliyopewa. Usiwaonee wengine wivu, lakini tembea katika upendo nao na uaminifu kwa mwito na neema iliyo juu ya maisha yako.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Wewe ni mtu wa ajabu aliye na karama na uwezo mwingi, na huhitaji kujilinganisha na mtu yeyote mwingine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon