Kaeni Ndani ya Mungu

Nyinyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote, nanyi mtatendewa (YOHANA 15:7)

Andiko la leo linatuambia tunaweza kuuliza chochote “tunachohiari” na tutafanyiwa tukikaa ndani ya Kristo. Njia ya pekee ambayo hili linawezekana ni sisi kuunganisha matamanio yetu na matamanio ya Mungu tunapozidi kukomaa ndani yake.

Lengo la kila aaminiye wa kweli ni kuwa mmoja na Mungu. Hili hufanyika kiroho tunapozaliwa upya, na hufanyika katika nia, hiari, na hisia tunapoendelea kukua na kukomaa ndani yake. Tunapofanya hivyo, matamanio yetu yanakuwa yake na tunakuwa salama katika kuyafuata.

Mwito ambao Dave na mimi tunao kwenye huduma yetu ni mfano mzuri. Matamanio ya Mungu yalikuwa kwetu sisi kuwa katika huduma na kusaidia watu karama alizotuneemesha nazo kuwasaidia. Hayo pia yamekuwa matamanio ya mioyo yetu. Tusingetumia wakati mwingi kwa kusafiri kila wikendi, kukaa mahotelini, na kuwa mbali na familia yetu iwapo matamanio yetu ya huduma yasingekuwa yametoka kwa Mungu. Ameweka msukumo wenye nguvu wa kuhudumu ndani yetu kiasi kwamba tunahiari kujitolea iwezekanavyo au kushinda vipingamizi ambavyo huenda vikaja kinyume nasi ili tukamilishe mapenzi yake kwetu.

Kukaa ndani ya Mungu ni “kushinda nje” naye, kutumia muda wetu naye, kuishi katika uwepo wake, na kukuza matamanio anayoweka katika mioyo yetu, kwa sababu hayo ndio mapenzi yake kwetu. Anazungumza nasi na kuweka matamanio katika mioyo yetu ili tuombe na kumwuliza vile vitu anavyotaka kutupatia. Atakuwa mwaminifu kutupatia matamanio yetu, bora yawe matamanio yake pia na bora tu tunakaa ndani yake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

“Shinda nje” na Mungu leo; Ni rafiki mkuu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon