Yesu alikuja kutuongoza katika njia ya amani

Yesu alikuja kutuongoza katika njia ya amani

Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.  Luka 1:79

Ninaamini kuwa amani ni mojawapo ya faida muhimu na baraka kubwa ambazo Mungu ametupa. Hata hivyo, katika shughuli za maisha ya kila siku na shinikizo linaloleta, mara nyingi tunahisi kitu chochote isipokuwa amani. Lakini haifai kuwa hivyo.

Luka 1:79 inasema kuwa moja ya mambo ambayo Mungu alimtuma Yesu kufanya ni kutuongoza katika njia ya amani. Kama waumini, tuna fursa nzuri ya kutembea katika amani ya Mungu isiyo ya kawaida, bila kujali shughuli zetu nyingi au nini kinachotuzunguka.

Niliishi miaka arobaini ya kwanza ya maisha yangu bila ya amani-na nilikuwa na huzuni. Hatimaye nilifikia hatua ya kuwa na shauku sana kwa ajili ya amani kiasi kwamba nilikuwa na nia ya kufanya kazi na Mungu kufanya mabadiliko yoyote yaliyotakiwa ili iwe nayo. Nashukru kwamba, sasa ninafurahia maisha ya amani ambayo mara nyingi hupita ufahamu. Ninaweza kutembea katika njia ya amani wakati wa dhoruba za maisha, si tu wakati dhoruba haipo.

Je! Umefanya uendelezaji wa amani kuwa kipaumbele? Mungu anataka ufanye hivyo. Mfuate Roho Mtakatifu ndani ya amani ambayo ni haki yako katika Kristo.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, asante kwa kumtuma Yesu “kuongoza na kuelekeza” miguu yangu katika amani Yako. Ninapokea baraka yako kubwa ya amani kwa maisha yangu

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon