Sisi sote tunapigana vita vizuri

Sisi sote tunapigana vita vizuri

Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.  Isaya 43:2

Ninaamini kwamba moja ya uongo ambao tunakabiliwa mara kwa mara ni kwamba tuko peke yetu tukipigana na shetani. Ibilisi anapenda kututenga na kutufanya tufikiri hakuna mtu mwingine anayepitia kile tunachopitia.

Uweli ni kwamba, sisi sote tunapigana. Sio wewe peke yako unayechoka. Sio wewe peke yako unayechoka  kusimama na kupinga uongo wa Shetani na hata kupinga hisia zako mwenyewe.

Mimi napigana vita vizuri vya imani kama vile unavyofanya. Na kuna waumini wengine ambao wamesimama pamoja na wewe dhidi ya adui.

Bora zaidi ni kwamba, Mungu yu pamoja nawe kila hatua ya njia. Isaya 43: 2 inaahidi kwamba tutafaulu kupitia nyakati za kujaribiwa kwa sababu Mungu mwenyewe ataenenda pamoja nasi. Tunapovuka katika maji, hawezi kutuacha, na wakati tunapitia kwenye moto, hatuwezi kuchomwa, kwa sababu Yeye yu pamoja nasi. Hivyo jipe moyo. Jizatiti. Mungu atakupa nguvu na hekima kwa vita vyote unavyokabili.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, asante kwa kuwa nami na kwa wafuasi wako wote ambao pia wanapigana dhidi ya adui. Siamini uongo ambao unasema mimi niko peke yangu. Wewe ni mwaminifu daima kuwa na sisi na kutusaidia wakati tunakuhitaji

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon