Huruma zake ni mpya kila siku!

Huruma zake ni mpya kila siku!

Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.  Maombolezo 3:22-23

Kila siku ni fursa mpya ya kufunga mlango juu ya siku za nyuma na kuwa na mwanzo mpya. Ukweli kwamba Mungu aligawanya siku katika makundi ya saa ishirini na nne ni ushahidi kwamba tunahitaji kuanza mara kwa mara. Daima kuna siku mpya, mwezi mpya na mwaka mpya. Lakini ili tufanye matumizi ya mwanzo huu mpya, tunapaswa kufanya uamuzi wa kufanya hivyo.

Je, unapigana na hatia na hukumu? Unajisikia vibaya kuhusu kitu ulichofanya miaka mingi iliyopita, au kitu kilichotokea jana? Haijalishi muda uliopita, siku za nyuma bado zimepita. Kitu kilichofanyika kilishafanyika, na Mungu peke yake ndiye anaweza kuitunza sasa. Sehemu yako ni kukubali kosa lako, kutubu, kupokea msamaha wa Mungu, na kuendelea.

Katika Maombolezo, nabii Yeremia anatuhimiza kwa habari kwamba huruma ya Mungu ni mpya kila asubuhi. Kila siku Anakupa mwanzo mpya. Ninafurahi kwamba Mungu anatuma kifurushi kipya cha huruma kila siku- tunaweza kuwa na mwanzo mpya kila siku!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ninafurahi sana kwamba huruma zako ni mpya kila asubuhi! Naweza kuanza upya kila siku kwa sababu ya upendo wako, huruma, rehema na uaminifu kwangu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon