Kamata Mbweha

Tukamatie mbweha, wale mbweha wadogo, waiharibuo mizabibu… —WIMBO ULIO BORA 2:15

Masikitiko madogo yanaweza kusababisha mfadhaiko, ambao hatimaye unaweza kuleta shida kubwa zaidi inayoweza kuzaa uharibifu mkubwa sana.

Kando na masikitiko makubwa yanayofanyika tunapokosa kupata kazi, kupandishwa cheo kazini, au nyumba tuliyotaka, tunaweza kuwa na hasira ndogo. Kwa mfano, je, iwapo unatarajia kukutana na mtu kwa chakula cha mchana kisha afike akiwa amechelewa. Ama labda ufanye safari maalum kwenda kwa duka kuu kununua kitu kilichopunguzwa bei halafu upate kishauzwa.

Aina hii ya masikitiko ni ndogo, lakini inaweza kukusanyika pamoja na kusababisha balaa. Ndiyo kwa sababu tunahitaji kujua jinsi ya kuyashughulikia na kuyaona yakija. La sivyo, yanaweza kutuzidi na kufanywa kuwa makubwa kuliko yalivyo.

Tutakuwa na busara kujikinga kutokana na mbweha wadogo wanaoiba amani yetu.

Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujifunza kufanya vile Paulo alifanya katika kitabu cha Matendo ya Mitume nyoka alipouzongazonga mkono wake—alimtukusa (Matendo ya Mitume 28: 1-5)! Tukijizoesha kukabiliana na masikitiko mara tu yanapotokea, hayatakusanyika na kuwa mlima wa uharibifu.


Ushindi sio kutokuwepo kwa matatizo; ni uwepo wa nguvu za Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon