
Basi ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu (1 WAKORINTHO 12:1)
Mengi yameandikwa kuhusu karama za Roho katika historia yote ya Wakristo. Biblia yenyewe inatufundisha kuhusu umuhimu wa wa karama za Roho na umuhimu wa sisi kukosa kuzipuuza. Ilhali mbali na habari zote zilizopo leo kuhusu mada hii, watu wengi hawazijui hizi karama kabisa. Mimi nilihudhuria kanisa kwa kipindi cha miaka mingi na sikuwahi kusikia mahubiri au funzo la aina yoyote kuhusu karama za Roho. Sikujua hata zilikuwa nini, acha hata kujua kwamba ningekuwa nazo.
Kuna aina nyingi za “karama” au “vipaji,” vile vinavyoitwa katika Biblia ya Amplified, ambayo pia inaviita “nguvu za kiajabu zinazowatofautisha Wakristo fulani” (1 Wakorintho 12:4). Hizo karama hutofautiana, lakini zote hutoka kwa Roho Mtakatifu. Tunapomwacha Mungu kutuongoza katika matumizi ya karama hizi, zinaongeza nguvu kiwango cha ajabu cha nguvu katika maisha yetu. 1 Wakorintho 12:8-10 inaorodhesha hizo karama ifuatavyo: neno la hekima, neno la maarifa, imani, karama za kuponya, kutenda miujiza, unabii, kupambanua roho, aina za lugha na fasiri za lugha.
Huu wote ni uwezo, karama, mafanikio na utajiri wa nguvu za kiungu ambazo aaminiye huwezeshwa kukamilisha kitu kisicho cha kawaida, na kila aaminiye anaweza kuzipata. Hatuwezi kulazimisha utumikishi wa karama yoyote ya kiroho. Tunafaa kutamani karama zote kwa bidii, lakini Roho Mtakatifu huchagua wakati na mtu ambaye zitatumikishwa. Muombe na utarajie uongozi wa Mungu kuhusu karama za Roho.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Si lazima uishi katika udhaifu kwa kuwa nguvu za Mungu ziko kwa ajili yako leo, na kila siku.