. . . Je? Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni, atawapa mema wao wamwombao. —MATHAYO 7:11
Kila mmoja wetu angependa kupewa kibali au kuwa maarufu. Je, hicho ni kiburi? Hapana, sio kama hilo linatoka kwa Mungu na sio kwa tamaa za kibinafsi au bidii zetu binafsi za kichoyo ili tutambuliwe.
Kwa kweli, huwa ninaona likiwa jambo la kufurahisha kwangu kutazama Mungu akimpa mtu umaarufu. Ni jambo la kufurahisha kumtazama akichagua mtu miongoni mwa wengi ili amshughulikie kwa njia maalum au kupendelea kumshughulikia. Kuona akifanya kazi katika maisha ya mtu kwa nguvu kuu huchochea sifa na shukrani za kweli.
Ni jambo la kufurahisha sana kuwa na kibali kwa Mungu. Inaonekana kwamba haifanyiki kila mara vile tungependa. Mojawapo ya shida ni sisi. Kuna mambo mengi sana ambayo Mungu angependa kutufanyia, lakini hawezi kwa kuwa hatujaomba. Sababu moja inayofanya tusiombe ni kwa sababu tunahisi kwamba hatustahili. Hakuna mmoja wetu anayeweza kustahili bila yeye lakini Mungu atatupatia kibali tukiomba!
Ni wakati wa kuamini kwamba Mungu anataka kutubariki. Anapenda kutupatia kibali chake. Kama mtoto wa Mungu aliyekombolewa, kusamehewa, na kupendwa, weka hili moyoni mwako leo: Wewe ni tunda la jicho la Mungu. Anakupenda!
Baba yetu wa mbinguni anataka wanawe wasimame wawe kila kitu ambacho Mwanawe Yesu Kristo alitwaa maisha yake ili wakawe.