Kitu ambacho Humvutia Bwana

Kitu ambacho Humvutia Bwana

Ili niitangaze sauti ya kushukuru, na kuzisimulia kazi zako za ajabu. ZABURI 26:7

Kutoa shukrani ni sehemu muhimu ya maombi kwa sababu kama sifa na ibada, ni kitu ambacho humvutia Mungu. Ni kitu ambacho Mungu hupenda, kitu ambacho huinua moyo wake. Wakati wowote tunapompendeza Mungu hivyo, undani wake naye huongezeka—na hilo huboresha maombi.

Pia, tukiwa wenye shukrani, tunakuwa katika nafasi ya kupokea zaidi kutoka kwa Bwana. Iwapo hatuna shukrani kwa kile tulicho nacho, kwa nini Mungu atupatie kitu kingine ili tulalamike na kunung’unika kukihusu? Kwa upande ule mwingine, Mungu akiona kwamba kwa kweli tunafurahia na kushukuru kwa kila kitu anachotupatia—vitu vikubwa na vitu vidogo—Analazimika kutubariki hata zaidi.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa ninaweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi nawe. Ninaomba shukrani zangu ziwe zikikubariki. Ninakupenda na ninashukuru kwa kila kitu ambacho umenipa, hata kiwe kidogo au kikubwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon