Kuachilia Uzito wa Wasiwasi

Kuachilia Uzito wa Wasiwasi

Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? MATHAYO 6:27

Ni kitu kimoja kujua kwamba hatufai kuwa na wasiwasi, lakini ni jambo jingine kushukuru kwa ajili ya ukweli huo na kwa kweli kuacha kuwa na wasiwasi. Mojawapo ya vitu ambavyo vilinisaidia kuacha wasiwasi ni mwishowe nilipotambua vile ni kitu kisichokuwa na maana kabisa. Hebu nikuulize: Umesuluhisha shida ngapi kwa wasiwasi? Je, kuna kitu ambacho kimekuwa kizuri zaidi kutokana na wasiwasi wako? Bila shaka hapana.

Mara tu ukianza kuwa na wasiwasi au kuhisi kufadhaika, mpe Mungu wasiwasi wako katika maombi. Achilia uzito wa wasiwasi huo na umwamini kikamilifu ili akuonyeshe la kufanya au akishughulikie mwenyewe. Maombi ni kani ya nguvu dhidi ya wasiwasi. Ninakumbushwa kuhusu wimbo wa zamani wa injili unaoitwa “Una wasiwasi wa nini ihali waweza kuomba?”
Unapokuwa chini ya mshinikizo, ni vizuri zaidi kuomba kuhusu mahitaji yako badala ya kuhangaika au kulalamika juu ya mahitaji hayo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba sihitaji kuishi maisha yaliyojaa wasiwasi. Ninakushukuru kwamba ninaweza kuja kwako kwa maombi wakati tu ninapoanza kuwa na wasiwasi kuhusu kitu na ninaweza kukupa mzigo wangu. Nisaidie kufanya uamuzi wa hekima wa kuacha kuwa na wasiwasi na kuanza kukuamini leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon