Shikilia Maisha ya Kuburudisha na Kusisimua

Shikilia Maisha ya Kuburudisha na Kusisimua

Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako. ZABURI 37:4

Ni vizuri kufanya kitu kisichotarajiwa mara mojamoja (au pengine kila mara) au kitu kipya au “kitu kisichozoelewa.” Fanya kitu ambacho kitashangaza watu na pengine kukuchemsha bongo kidogo. Itafanya maisha yako yasisimue, na utaishia kumshukuru Mungu kwa changamoto au vituko vyako vya kusisimua.

Hatujaumbwa na Mungu kufanya kitu kimoja mara kwa mara hadi kikose maana. Mungu ni mbunifu. Tazama tu tofauti zilizopo katika vitu vyote alivyoumba na utakubali kuwa ubunifu wake hauna mwisho.

Iwapo hujatambua, Mungu hubadilisha vitu mara kwa mara katika maisha yetu. Usiogope mabadiliko. Anza kufanya baadhi ya vitu ambavyo ungependa kufanya lakini ambavyo umekuwa ukisitisha kufanya kwa sababu hujawahi kuvifanya.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba unaburudisha na kusisimua maisha yangu. Kila siku ni changamoto mpya na matukio tofauti. Ninakushukuru kwamba ninaweza kusisimka kuhusu mustakabali ulio mbele yangu na ninaweza kuishi maisha mapya, yenye ujasiri, na ubunifu ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon