Kuchagua Kuwaza kwa Njia Chanya

Kuchagua Kuwaza kwa Njia Chanya

Mungu fikra zako zina thamani nyingi kwangu; jinsi ilivyo kubwa jumla yake! ZABURI 139:17

Mtu jasiri ana mtazamo chanya wa maisha. Ujasiri na mtazamo hasi haviendi pamoja. Ni kama mafuta na maji; havichanganyiki tu. Nilikuwa mtu mwenye mtazamo hasi sana, lakini, shukuru Mungu, alionyesha kwamba kuwa mtazamo chanya huburudisha na kuzaa matunda mengi.

Wanapohimizwa kuwa na fikra chanya, mara nyingi watu hujibu kwa ukali, “Hilo haliwezekani.” Lakini imesemwa kuwa asilimia 90 ya mambo tunayokuwa na wasiwasi nayo huwa hayafanyiki. Kwa nini watu huchukulia kwamba, inawezekana kuwa na fikra hasi kuliko kuwa na fikra chanya?

Kuwaza mawazo chanya ni jambo rahisi na hutegemea iwapo tunataka kutazama mambo kwa mtazamo wa Mungu au wa Shetani. Je, unapowaza, huwa unadhamiria kuchagua kuwaza fikra chanya za shukrani—au unawaza tu kwa utulivu kila mawazo yanayotupwa katika nia yako? Ukiwa mawazo hasi, utakuwa na dhiki. Kwa nini uwe na dhiki ilhali unaweza kuwa na furaha.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba ninaweza kuchagua fikra nitakazotafakari. Kwa usaidizi wako ninaweza kukataa kuwaza mawazo hasi, na kutafakari kwa misingi ya neno lako. Asante kwa kuwa ninaweza kuwa mtu jasiri, aliye na mtazamo chanya wa maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon