Kuchelewa sio Kukana

Nyakati zangu zimo mikononi mwako; uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia (ZABURI 31:15)

Tunapoomba, hatupati majibu ya maombi yetu moja kwa moja. Wakati mwingine inatubidi kungoja muda mrefu, lakini hiyo haimaanishi kwamba Mungu anasema hapana kwa maombi yetu. Ni muhimu sana kuamini wakati wa Mungu katika mambo yote yanayotuhusu sisi na maisha yetu. Pengine umekuwa ukingoja kupata upenyo katika kitu ambacho umekuwa ukiombea kwa muda mrefu, na kimya cha Mungu kimeleta hali ya kuchanganyikiwa katika maisha yako. Tafadhali kumbuka kwamba Mungu si mwanzilishi wa ghasia. Anataka umwamini sio kuchanganyikiwa.

Kuchelewa kwingi huwa ni kwa kiungu. Huwa kumepangwa na Mungu ili kufanya kazi ambayo inafaa kufanywa ndani yetu. Tukiendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu hata katika nyakati za giza tunaanza kuwa na tabia za kiungu zilizoimarika. Fikiria kuhusu Yusufu, aliyengoja kwa muda wa miaka kumi na mitatu ili kuona majibu ya maombi yake; au Ibrahimu, aliyengoja kwa muda wa miaka ishirini. Wangalisalimu amri, wasingalifurahia matunda ya imani yao ndani ya Mungu. Huenda Mungu asije mapema lakini hatachelewa. Vitu vingi tunavyofaa kuwa navyo huchukua muda mrefu kuja kuliko tulivyofikiria, na huwa vigumu kuvisubiria. Lakini Mungu anajua haswa anachofanya na anataka ungoje muda wake.

Mungu hutuahidi kutuokoa kutoka kwa maadui zetu, lakini tunapoendelea kungoja tunahitaji kuwa tunawaombea na kuwa baraka kwa watu iwezekanavyo. Mungu anafanya kazi huku ukingoja!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jifunze kungoja kwa amani au muda mrefu wa maisha yako utakuwa wenye dhiki.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon