Wakati Mwingine Unahitaji tu Kuchukua Hatua

Wakati Mwingine Unahitaji tu Kuchukua Hatua

Nathani akamwambia mfalme, haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako, maana Bwana yu pamoja nawe. —2 SAMWELI 7:3

Je, kuna kitu ambacho unatamani kufanya, lakini umekuwa ukingoja? Je, Mungu ameweka kitu moyoni mwako lakini ukawa unasita kuchukua hatua?

Ninaamini wakati wa Mungu ni muhimu sana, na bila shaka sifikirii tunafaa kuharakisha chochote bila kuomba kukihusu na kupata ushauri mzuri wa kiungu. Hata hivyo, nimegundua watu wengine huishi maisha wakiwa wamekwama katika “hali ya kungoja.” Wanangoja wakati ule wanagekuwa wanachukua hatua katika imani.

Hakuna kitu kinachofadhaisha kuliko kujishughulisha kila siku na kufika tu mwisho wa siku, wiki, mwezi, au mwaka na kuhisi kwamba hauko hata karibu kufikia ndoto au lengo lako. Mungu hataki uishi katika mfadhaiko huo. Anataka utafute mapenzi yake, halafu uchukue hatua ya kujishughulisha. Ukimkosa Mungu—ukichukua hatua kuelekea upande mbaya—Mungu atakuregesha kwa njia.

Ni nia ya moyo wako iliyo muhimu. Mungu hupendezwa akiona kwamba unachukua hatua kwa imani, kujaribu kumpendeza na kutimiza mapenzi yake juu ya maisha yako. Kwa hivyo usihofu leo. Chukua hatua na utazame Mungu akianza kufanya kazi ndani ya maisha yako. Kinachojalisha ni nia ya moyo.


Mungu ataweka matamanio ndani ya moyo wako na atakusaidia kuyatimiza. Kazi yako ni kutumia tu imani yako kuchukua hatua kuelekea kwenye lengo hilo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon